Numbers 32:32-37

32 aTutavuka mbele za Bwana kuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ng’ambo hii ya Yordani.”

33 bKisha Musa akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yusufu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.

34 cWagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri, 35 dAtroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha, 36Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo. 37 eNao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu,
Copyright information for SwhKC